Serikali kuchunguza kifo cha mwanafunzi Bombo – Tanga

Serikali imesema inachunguza Taarifa Kuhusu Kifo Cha Mwanafunzi Wa Shule Ya Sekondari Ya Maweni Anayedaiwa kufariki kwa Uzembe Wa Madaktari Na Manesi Wa Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa wa Tanga.

Serikali Ya Mkoa Imesema Imetuma Timu Za Uchunguzi Ikiongozana Na Mganga Mkuu Wa Mkoa Kuchunguza Madai Hayo Pamoja Na Mengine Yanayosambaa Yakiwemo Ya Mtoto Mchanga Kuvunjika Mkono Wakati Mjamzito Akijifungua Katika Hospitali Ya Mji-Korogwe -Magunga.

Taarifa Ya Mkuu Wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini, Jamali Zuberi Imeeleza Kuwa Ikibaini Kuna Uzembe Katika Matukio Hayo, Adhabu Za Kitaaluma Au Jinai Zitachukuliwa Itakapobidi Kufanya Hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *