Serikali Ipo Tayari Kupokea Ushauri Katika Hili

Na Gideon Gregory,Dodoma

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema Serikali ipo tayari kupokea ushauri utakaowezesha kuboresha usalama wa matumizi ya mtandao hapa nchini.

Mha. Mahundi ameyasema hayo leo Mei 27,2024 Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Mussa Salimu Mbunge wa Gando aliyetaka kujua Serikali haioni haja ya kuhamishia Mfumo wa Cyber kuwa chini ya udhibiti wa Jeshi la Polisi.

Amesema mkakati wa Taifa wa Usalama umeweka malengo na mpango wa kimkakati wa nchi kuhakikisha ulinzi na usalama wa anga ya mtandao (cyber space).

“Ndani ya Mkakati huo, Taasisi zote zinazohusika na ushughulikiwaji wa makosa ya mtandao zimetambuliwa na majukumu yao kuwekwa bayana ili kuwepo utaratibu mzuri wa kushirikiana”, amesema.

Pia ameongeza kuwa suala la ushughulikiwaji wa anga ya mtandao (cyber) ni mtambuka na haliwezi kutekelezwa kwa ufanisi na Taasisi moja hivyo ni muhimu Taasisi hizo ziendelee kutekeleza usimamizi huo kwa kushirikiana na kwa utaratibu jumuishi ili kuongeza tija katika jukumu hilo. Haya funguka,unaishauri nini Serikali katika suala zima la Usalama Mtandaoni

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *