SERIKALI INATAMBUA MCHANGO WA TAASISI ZA ELIMU KATIKA KULETA MAENDELEO – RC MTANDA

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na kusema Serikali inatambua mchango wa taasisi za elimu nchini katika kuleta maendeleo.

Katika kikao hicho cha Agosti 19, 2026, uongozi wa chuo ulimueleza Mkuu wa Mkoa kuhusu maendeleo ya chuo hicho pamoja na hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi inayoendelea ndani ya Mkoa wa Mwanza.

Akizungumza baada ya kikao hicho, RC Mtanda ameuahidi uongozi wa chuo kuwa Serikali ya Mkoa ipo tayari kutoa ushirikiano unaohitajika, ili kuhakikisha shughuli na miradi ya chuo hicho inatekelezwa kwa ufanisi na kwa kuzingatia malengo yaliyowekwa.

Amesema, kwa kuwa Serikali inatambua mchango wa taasisi za elimu katika kuleta maendeleo, ipo tayari kushirikiana kwa karibu na kwamba miradi ya ujenzi inayotekelezwa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania katika Mkoa wa Mwanza imefikia wastani wa asilimia 73.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *