Msanii wa muziki na muigizaji wa filamu, Selena Gomez ametangaza rasmi kujiondoa kwenye mitandao ya kijamii.

Selena, ambaye anawafuasi zaidi ya Milioni 430 kwenye mtandao wa Instagram, amesema hayo jana Alhamis, huku akitaja sababu ya kujitoa ni “moyo wake unaumia kuona mambo ya kutisha, chuki, vurugu na ugaidi unaoendelea duniani,” ikiwemo kile kinachoendelea katika ukanda wa Gaza ambapo kuna vita vya Israel na kundi la Hamas (Palestina)
