Kwa mujibu wa mitandao wa Untamed Travelling umetaja sehemu za kuvutia nchini Tanzania ambazo ukienda utaacha histori nzuri na ya kupendeza maishani mwako.
Sehemu hizo ni Hifadhi ya Serengeti, Zanzibar, Nungwi, Kilimanjaro, Mnembe, Hufadhi ya Wanyama Ruaha, Mafia, Ziwa Manyara, Hifadhi ya Ngorongoro na Milima ya Mahale.
Sehemu kama Hifadhi ya Serengeti ni eneo kubwa la mbuga na misitu kaskazini mwa Tanzania hasa katika mikoa ya Mara na Arusha, Eneo lake ni linaukubwa wa 14,763 km².
Zanzibar inabeba na kisiwa cha Nugwi na Mnembe, na Zanzibar iimebarikiwa kuwa na fukwe nyingi na nzuri za bahari na hoteli zaidi ya 50 kwenye kisiwa hicho. Kisiwa hicho kinatajwa kuwa na ukubwa wa 2,461 km².
Mlima Kilimanjaro nao pia umetajwa kuwa sehemu ya kivutia ambapo mlima huu upo Mkoa wa Kilimanjaro. Una urefu wa mita 5,895. Hali halisi Kilimanjaro ni zaidi ya mlima tu, ni kama safu ndogo ya milima mitatu: Kibo, Mawenzi na Shira.
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ni hifadhi ya Tanzania. 2008 inaukubwa takriban kilomita za mraba 20,226 (sq mi 7,809).
Hifadhi hii iko takriban kilomita 130 (81 mi) magharibi mwa Iringa. Hifadhi hii ni sehemu ya eneo la kilomita za mraba 45,000 (sq mi 17,000).
Hifadhi ya Ngoro ngoro ni Sakafu ya kreta iko mita 1,800 (futi 5,900) juu ya usawa wa bahari. … Kreta imekuwa miongoni vivutia vikubwa Duniana na imeingia hadi kwenye Maajabu Saba ya Asili ya Afrika.
Ziwa Manyara ni moja kati ya maziwa ya Tanzania,Ni la saba kwa eneo. Ukubwa wake ni Km² 470. Kina chake hakizidi mita 3.7. Linapatikana kaskazini mashariki, katika Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara.