SAUDI ARABIA YASHINDA TENDA YA KUANDAA KOMBE LA DUNIA 2034.

Shirikisho la Soka Duniani FIFA, limethibitisha kuwa Kombe la Dunia la mwaka 2034 litafanyika Nchini Saudi Arabia baada ya kushinda zabuni ya uandaaji wa mashindano hayo makubwa ya Dunia, ambapo hiyo itakuwa mara ya kwanza Kombe la Dunia kufanyika katika Nchi moja pekee tangu idadi ya Timu ilipoongezwa hadi kufikia 48.

FIFA imethibitisha kuwa Kombe la Dunia la 2034 litafanyika Saudi Arabia, wakati Kombe la Dunia la 2030 litaandaliwa kwa ushirikiano wa Uhispania, Ureno na Morocco na mechi tatu za ufunguzi zitachezwa Amerika Kusini.

Saudi Arabia iliibuka mwaka jana kama mzabuni pekee katika mchakato wenye utata ambao ulishuhudia FIFA ikichanganya maamuzi ya mashindano ya 2030 na 2034 kuwa kura moja, ikimaanisha kuwa wajumbe waliunga mkono au kupinga zabuni zote mbili bila kura tofauti.

Saudi Arabia imekosolewa kwa ukiukaji wake wa haki za binadamu, kuharamisha mapenzi ya jinsia moja, vizuizi vya uhuru wa kusema na ukosefu wa haki za wanawake, Nchi hiyo itakuwa mwenyeji wa mashindano ya hadhi ya juu zaidi ya mpira wa miguu kwa mara ya kwanza na ni mfano wa hivi punde wa ushawishi unaokua wa Saudi Arabia kwenye michezo ya kimataifa.

Saudi Arabia ilikabidhiwa fainali kwa makubaliano yaliyofikiwa katika kikao cha Baraza la FIFA kilichokaa Oktoba mwaka jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *