Saudi Arabia itashiriki shindano la Miss Universe mwaka huu

Mrembo Rumy Alqahtani(27) atakuwa mshiriki wa kwanza kutoka nchini Saudi Arabia, ambaye atashiriki shindano la Miss Universe mwaka huu na ni kwa mara ya kwanza nchi hiyo.

Alqahtani ni mwanamitindo ambaye ana shahada ya kwanza ya udaktari wa meno.

Mashindano ya mwaka huu yatafanyika Mexico na pia yatajumuisha pia nchi ya Iran.

“Nimejivunia kushiriki shindano la Miss Universe 2024. Huu ni ushiriki wa kwanza wa Ufalme wa Saudi Arabia katika shindano la Miss Universe,” Alqahtani ameandika kwenye akaunti yake ya Instagram mapema wiki hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *