Na Afaraha Suleiman, Babati – Manyara.
Mgombea Urais kwa tiketi ya Sauti ya Umma (SAU), Majalio Paul Kyara amesema endapo watapewa ridhaa na Wananchi kushinda uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 watatoa ajira kupitia sekta ya Kilimo kwa kuboresha mashamba ya uwekezaji yaliyopo wilayani Hanang’ Mkoani Manyara.
Kyara ametoa ahadi hiyo akiwa kwenye mwendelezo wa kunadi sera na ilani ya chama hicho mjini Babati, wakati akiwahutibia Wafanyabishara wa soko kuu la mji huo.

Aidha, amesema licha ya kuboresha sekta ya kilimo lakini pia wataboresha sekta ya elimu na ujenzi wa soko la kisasa la mjini wa Babati, ili kuondoa msongamano kwenye soko hilo.



