‘SANGOMA’ KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MAMA YAKE GEITA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, limemfikisha Mahakamani Mganga wa Kienyeji na mkazi wa kijiji cha Rutunguru, Lufuta Magoma (40), akikabiliwa na tuhuma za mauaji ya mama yake mzazi, Dotto Magoma Nyara (70).

Magoma amepandishwa kizimbani hii leo Julai 10, 2026, katika Mahakama ya Wilaya ya Chato na kusomewa shauri hilo la jinai namba 15471 la mwaka 2026, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Chato, Erick Kagimbo,.

Katika shitqka hilo, Wakili wa Serikali, Mashaka Said aliieleza Mahakama kwamba mshtakiwa alitenda kosa hilo Juni 4, 2026 katika Kijiji cha Rutunguru, kilichopo Wilaya ya Geita.

​Alidaiwa kumshambulia na kumuua Mama yake mzazi kinyume na kifungu cha 196 na 197 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2023.

​Akiwa Mahakamani, Mshtakiwa huyo hakutakiwa kujibu chochote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kisheria ya kusikiliza mashauri ya mauaji, ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 23, 2026.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *