Samatta aomba kutojumuishwa kwenye kikosi kilichoitwa kwa michezo ya FIFA Series 2024.

Nahodha wa Timu ya Taifa “Taifa Stars”, Mbwana Samatta ameomba kutojumuishwa kwenye kikosi kilichoitwa kwa michezo ya FIFA Series 2024.

Samatta amezungumza na Kocha kabla ya kutajwa kwa kikosi hicho na kuomba asijumuishwe katika safari hiyo ya Azerbaijan, ombi ambalo limekubaliwa.

Kikosi hicho kitakachoingia kambini Machi 17, 2024 kitaondoka Machi 18, 2024 na kitacheza michezo miwili na Bulgaria na Mongolia, michezo itakayochezwa Machi 22 na Machi 25, 2024.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *