Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Samatta ajiunga na Paok FC ya Ugiriki

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Ally Samatta amejiunga na klabu ya PAOK FC inayoshiriki ligi kuu nchini Ugiriki, kwa uhamisho huru akitokea Fenerbaçe ya Uturuki.

Samatta (30) amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu hiyo ambayo ilimalizika nafasi ya nne msimu uliopita ambapo sasa inawania nafasi ya kucheza Europa Conference league dhidi ya Beitar Jerusalem.

Samatta alijiunga na Fenerbaçe akitokea Aston Villa mnamo Septemba 2020 kwa mkopo na baadaye Julai 2021 akajiunga jumla kabla ya kucheza kwa mkopo kunako klabu ya Royal Antwerp msimu wa 2021-2022 na baadaye Genk ya Ubelgiji kwa mkopo pia msimu uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *