SALOME MAKAMBA ATINGA NA BAISKELI KUCHUKUA FOMU YA UBUNGE SHINYANGA.

NA EUNICE KANUMBA –SHINYANGA 

LEO  ikiwa ni siku ya pili tangu kufunguliwa kwa pazia  la uchukuaji wa fomu za watia nia wa nafasi za ubunge na udiwani  kwa chama cha mapinduzi, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Shinyanga Salome Makamba amechukua fomu kuomba kuteuliwa kugombea ubunge kuwakilisha wanawake (viti maalumu) kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Makamba amekabidhiwa fomu hiyo leo Jumapili, Juni 29, 2025 na Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Shinyanga Habiba Musimu.

Akiwasili katika ofisi hizo makamba ametumia usafiri wa baiskeli ambao ni hutumika zaidi katika jamii ya wasukuma kama nyenzo ya usafiri,  huku akiomba dua za watanzania ili aweze kuteuliwa kuwania nafasi hiyo  ili  kuendeleza gurudumu la kuwatumikia wanashinyanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *