Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Salah kuzikosa mechi mbili za Afcon kutokana na jeraha

Nyota wa timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah atazikosa mechi mbili za michuano ya kombe la mataifa ya afrika kutokana na jeraha la msuli wa nyuma ya paja.

Shirikisho la soka la Misri limesema kuwa Salah anayechezea pia klabu ya Liverpool nchini Uingereza, hatopatikana katika michezo miwili ijayo hadi hatua ya robo fainali.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, alitoka uwanjani mwishoni mwa kipindi cha kwanza katika mechi dhidi ya Ghana siku ya Alhamisi iliyokamilika kwa sare ya 2-2.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *