Tatizo la tumbo kujaa gesi imekuwa kubwa kwa siku za hivi karibuni. Hii inatokana nalishe mbovu tunayokula kila siku kwa kutegemea zaidi vyakula vya haraka na bei rahisi (fast foods & snacks). Vyanzo vingine vya tatizo ni msongo wa mawazo, matumizi ya vidonge mara kwa mara na mazingira yenye sumu yanayotuzunguka kama moshi wa magari na kemikali za viwandani.
Hizi ni Sababu 8 zinazosababisaha tumbo Tumbo Kujaa Gesi
Matatizo kwenye Mmeng’enyo wa Chakula
Magojwa kama Ulcerative colitis, celiac disease na IBS-inflammatory bowel syndrome huletekeza kujaa gesi kwa tumbo
Maji kubakizwa mwilini (fluid retention)
Wakati fulani maji yanaweza kuabakizwa kwenye sehemu fulani za mwili kama kweye magoti, tumboni na kwenye nyonga. Maji haya huletekeza maumivu makali kwenye joints na tumboni. Uwepo wa maji tumboni hujulikana kama ascites na inaweza kuashiria kwamba una tatizo kwenye ini au maambukizi ya bacteria.
Ndio maana kuna umuhimu wa kufanya vipimo kama una homa ya ini (hepatitis B). kama kuna shida ya ini basi utapata dalili zingine kama kichfuchefu, macho na ngozi kuwa njano, kupungua uzito, kutapikadamu na chakula kutosagwa tumboni.
Mwili kukosa maji (Dehydration)
Umewahi kufuatilia siku ukiwa umekunywa sana pombe ama kula zaidi vyakula vyenye chumvi kwa wingi na tumbo likajaa gesi?. Mwili unapokosa maji hufanya uchakataji na usagaji wa chakula kuwa mgumu. Mwili unapokosa maji ya kutosha hufanya kazi ya kuvuta na kuhifadhi maji mengi zaidi pale utakapokunywa maji ili kuepuka kutokea kwa upungufu huu. Maji yanapokuwa mengi kupita kiasi ndipo sasa unaweza kupata choo kigumu ama kukosa choo. Hakikisha unakunywa maji mara nyingi zaidi kila siku ili kuepuka tumbo kujaa gesi.
Kukosa choo ama kupata choo kigmu/Constipaton
Constipation inaweza kuwa sababu kubwa ya kwanini tumbo lijae gesi. Constipation inaweza kusababisha choo kigumu, maumivu tumboni na kukosa choo kwa muda mrefu. Kukosa choo na choo kigumu husabishwa na ulaji wa vyakula vilivyokobolewa sana visivyo na kambakamba, matumizi kidogo ya maji, msongo wa mawazo na kuishi bila kufanya mazoezi.
Alegi ya Chakula
Alegi ya vyakula mbalimbali kama maziwa, mayai na ngano vinaweza kuwa ni sababu ya kujaa gesi kwa tumbo lako. Kuna aina nyingi ya vyakula inaweza kusababisha upate mzip ama alegi. Cha kufanya sikiliza mwili wako unasemaje pale unapokula chakula. Kama mwili unakataa aina fulani ya vyakula na unapata mcharuko kama kuvimba, kuharisha, ama kutapika basi usitumie chakula hicho.
Maambukizi
Kama mwili unapambana na maambukizi aidha ya bacteria, virusi, fangasi au vimelea wengine basi utapata tatizo la kujaa gesi tumboni kutokana na mpambano wa ugonjwa na seli nyeupe za damu.
Majeraha Kwenye Mfumo wa Chakula
Wakati mwingine unaweza kupata gesi tumboni kutokana na vidonda ama uvimbe kwenye baadhi ya sehemu za mfumo wa chakula kama utumbo mdogo na utumbo mpana. Uvimbe unaweza kuzuia utolewaji wa uchafu na kuletekeza gesi na maji kukwama.
Mabadiliko ya Homoni
PMS (pre menstrual syndrome) ikimaanisha mkusanyiko wa dalili zisizo za kawaida za kipindi cha hedhi ni chanzo cha tumbo kujaa gesi. Tatizo linaweza kuwa kubwa kama una uvimbe kwenye kizazi na hedhi yako inavurugika. Kwanini wanawake hupata gesi tumbo wakati au karibia na kipindi cha hedhi? Mwanamke anapokaribia hedhi kiwango cha homoni ya estrogen huongezeka na ukuta wa mfuko wa mimba kuongezeka. Pale anapopata siku zake basi damu na maji mengi hutolewa nje na hivo tumbo kurudi katika hali ya kawaida.
Saratani
Moja ya dalili za saratani ya utumbo mpana na saratani ya mfuko wa mimba ni tumbo kujaa gesi. Ndio maana ni muhimu kuongea na daktari wako pale ambapo umejaribu kila njia ya kundoa tatizo lako lakini bado halijaisha.
Chanzo: Linda Afya