RUWASA MANYARA YAKABIDHI MIKATABA KWA WENYEVITI CBWOS

Na Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Meneja wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) Mkoa wa Manyara James Kionaumela amekabidhi mikataba ya Framework Agreement kwa wenyeviti wa vyombo vya watumia maji CBWO’s katika wilaya zote tano za mkoa Manyara, kufuatia kupatikana kwa wazabuni watakaotekeleza kazi hiyo katika kanda.

Katika hafla ya makabidhiano hayo kionaumela amewataka wenyeviti hao, kushirikiana kwa karibu na wazabuni hao ili kuhakikisha huduma ya maji inakuwa endelevu na kuepusha changamoto ya kusuasua na kusimama kwa huduma hiyo kwa wananchi.

“Hatua hii ni muhimu katika kuimarisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa mkoa wa Manyara”alisema Kionaumela

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *