Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Rutto akataa kuongezewa mshahara

Rais wa Kenya William Ruto, ametupilia mbali pendekezo la Tume ya Mishahara na Marupurupu nchini humo (SRC), iliyotaka kuongeza mishahara ya maafisa wakuu serikali akiwemo Rais Ruto na Naibu wake, na kuiagiza Tume hiyo kubuni mbinu za kusawazisha mishahara kwa maafisa wa serikali ili kuendana na viwango vya kimataifa.

Rais Ruto ametoa kauli hiyo wakati akizindua huduma za kidijitali za serikali, ambapo amewataka maafisa hao kusubili kwani haiwezekani watu wa ngazi za juu wapate mara 100 ya watu wa ngazi ya chini wakati wote wanaishi nchi moja.

Ikumbukwe kuwa, Tume hiyo ilipendekeza mshahara wa Rais uongezwe kutoka Ksh.1,433,750 (Tsh.24,626,644.62) hadi Ksh.1,650,000 (Tsh.28,341,038.27) na ule wa naibu rais kutoka Ksh.1,227,188 (Tsh.21,078,655.80) hadi Ksh.1,402,500 (Tsh. 24,089,882.53).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *