Rais wa Kenya, William Ruto, ametoa wito wa maridhiano na pole, huku akiomba radhi kwa Vijana wa Kenya na nchi jirani za Tanzania na Uganda.
Akizungumza wakati wa maombi ya kitaifa yaliyofanyika jijini Nairobi Mei 29, 2025 Rais Ruto pia alikiri Vijana wa Kenya kuchukizwa na matukio yaliyotokea mwaka 2024.

Aidha, Ruto pia aliomba radhi kwa Serikali ya Tanzania, hatua inayokuja baada ya siku chache tangu Martha Karua na jaji mku mstaafu wa Taifa hilo Willy Mutunga, wakamatwe na kufukuzwa walipojaribu kuingia Tanzania.