
Baada ya Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) kusema bondia wa ngumi za kulipwa, Karim Mandonga hatoshiriki ngumi mpaka atakapopimwa afya yake, majibu ya kipimo yametoka leo Agosti 15 baada ya kupimwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili yameonesha hana tatizo lolote la kiafya, hivyo anaruhusiwa kucheza pambano la Agosti 27 Visiwani Zanzibar.
Hayo yamethibitishwa na Khadija Muchenyi ambaye ni daktari na mjumbe wa kamati ya utendaji ya TPBRC.