RUKSA KUINGIA KENYA BILA VISA, WANACHAMA EAC WAPENDELEWA

Raia wa nchi zote Afrika isipokuwa Somalia na Libya sasa wataingia Nchini Kenya bila Visa, ambapo sasa kwa Nchi zilizopata msamaha huo raia wake wataruhusiwa kukaa kwa miezi isiyozidi miwili Kenya.

Taarifa kutoka Nchini humo imeeleza kuwa Nchi hizo mbili zimezuiliwa kutokana na sababu za kiusalama na Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wao wataruhusiwa kukaa hadi miezi sita.

Hatua hiyo, inalenga kuunga mkono ukuaji wa utalii na kukuza ushirikiano wa kikanda ikiwemo kurahisisha usafiri katika bara zima la Afrika unayisukumwa na Umoja wa Afrika.

Kenya sasa inaingia kwenye orodha ya nchi za Afrika ambazo zimeruhusu kusafiri bila visa ikiwemo Ghana, Rwanda, Senegal, Uganda, Shelisheli, Benin na Gambia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *