
Bunge limeazimia vijana wote wapewe fursa sawa katika ajira pale ambapo wamekuwa wametimiza masharti mengine yote yanayohusika na nafasi ya ajira husika isipokuwa cheti cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) hadi pale ambapo serikali itakuwa na uwezo wa kuwapokea vijana wote wanaomaliza kidato cha 4 na cha 6.
Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson ameyasema hayo leo Februari 16, 2024 bungeni mjini Dodoma wakati akiahirisha shughuli za Bunge la 12.


