Rufaa Yagonga Mwamba,Vybz Kartel Kuendelea Kusota Gerezani

Rufaa ya msanii wa muziki wa dansi Vybz Kartel ya kuachiliwa kwa dhamana yatupiliwa mbali na mahakama kuu ya Jamaica na msanii huyo ataendelea kusalia gerezani hadi Juni 10 wakati uamuzi juu ya hukumu yake utatolewa na Mahakama ya Rufaa,Kartel alihitaji kuachiliwa kwa dhamana baada ya hukumu yake ya mauaji kubatilishwa mwezi Machi mwaka huu.

Nyota huyo wa muziki wa dansi mwenye umri wa miaka 48, amekuwa gerezani nchini Jamaica tangu mwaka 2011 kutokana na kutoweka kwa mshirika wake Clive “Lizard” Williams, ambaye mwili wake haujawahi kupatikana.

Baada ya kesi ya siku 65, moja ya muda mrefu zaidi katika historia ya Jamaika, Kartel na wengine watatu walihukumiwa mwaka 2014. Kartel alihukumiwa kifungo cha maisha kwa kifungo cha chini cha miaka 35, na baadaye kupunguziwa kifungo baada ya kukata rufaa hadi miaka 32 na nusu.

Hukumu ya Kartel ilibatilishwa miezi miwili iliyopita,rufaa yake iliyofanikiwa na kusikilizwa na Baraza la Privy huko London, ilidai kuwa jaji anayetuhumiwa kujaribu kuwahonga wengine alipaswa kutupwa mbali na kesi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *