Rs Berkane Yagoma Kucheza Kisa Jezi

Mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup) kati ya  USM Alger ya Algeria na RS Berkane  ya Morocco  haujafanyika baada ya wageni RS Berkane kuzikataa jezi walizozikuta kwenye vyumba vya uwanjani wakidai sio zao.

Awali RS Berkane walidai jezi zao zilizuiwa Uwanja wa Ndege walipowasili Algeria, wakawaambia hawataruhusiwa kuzitumia kwa kuwa zina bendera ya Morocco, jambo ambalo lilipingwa na RS Berkane, wakasisitiza wanataka kuzitumia jezi hizo la sivyo hawataingia uwanjani kucheza.

Imeelezwa kuwa Msafara wa RS Berkane ulipofika vyumbani ukakuta jezi ambazo hazina bendera ya Morocco na hivyo wakagoma kuingia uwanjani, baada ya majadiliano marefu wakaondoka uwanjani.

Macho na masikio ya wadau wa soka hivi sasa ni ndani ya  Shirikisho la Soka Afrika CAF ili kufahamu uamuzi utakaochukuliwa kuhusiana na na kisa hiki kinachochagizwa na kutokuwapo kwa uhusiano mzuri wa  Kidiplomasia kati ya Algeria na Morocco na hicho kinatajwa kuwa chanzo cha Algeria kukataa uwepo wa Bendera ya Morocco kwenye jezi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *