Cristiano Ronaldo ameshinda kesi yake dhidi ya Juventus kuhusu mgogoro wake wa mshahara aliyokuwa ameikatia rufaa katika mahakama ya Usuluhishi nchini Italia.
Juventus italazimika kumlipa Ronaldo Euro Milioni 9.7 milioni kama mshahara wa nyuma wa msimu wa 2020-21 mahakama ya Italia ilitangaza Jumatano.
Jumla hiyo inalingana na tofauti kati ya mshahara aliopokea Ronaldo na ule ambao alipaswa kupokea baada ya kukatwa kodi na makato mengine.
Ronaldo, ambaye alikaa Italia kwa misimu mitatu akiwa na Juventus (2018-21) kabla ya kujiunga na Manchester United (2021-22) na kisha klabu ya Al Nassr ya Saudia, alikuwa akidai Euro milioni 19.5 lakini jopo la usuluhishi lilipunguza fedha hiyo kwa asilimia 50.