Rais wa Marekani, Donald Trump na Mkewe Melania Trump walilazimika kuondolewa kwenye hqfla ya Chakula cha jioni, baada ya kuripotiwa milio ya risasi kwenye majengo ya Hoteli.
Idara ya Siri ya Marekani ilithibitisha kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo la milio ya risasi, huku mtu mmoja Cole Allen (31), ametiwa mbaroni.

Katika hotuba yake aliyoitoa akiwa Ikulu ya White House, rais Trump alisema “inashangaza kila wakati hii inapotokea, hali ambayo haibadiliki”.
Aidha, mara baada ya tukio hilo, Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Kijamii kuwa, “Mpiga risasi amekamatwa, na nimependekeza kwamba “TUACHE SHOW IENDELEE” lakini, tutaongozwa kabisa na Utekelezaji wa Sheria.”

Hata hivyo Trump amesema vyombo vya sheria ndivyo vilimtaka yeye na mke wake kuondoka katika eneo hilo.
