Baby mama wa A$AP Rocky, Rihanna mapema wiki hii amefunguka kuhusu uzazi na kulea watoto, huku akionyesha kushangazwa na sura ya mmoja ya watoto wake.

Katika mazungumzo aliyofanya na Access Hollywood, mrembo huyo alionyesha kushangaa mtoto wake mkubwa Raz kurithi paji la uso wake(Komwe) na mdogo Riot kutokuwa na komwe.
“Kitu pekee ninachoweza kufikiria ni paji la uso la RZA, ambalo Riot haina!,” amesema staa huyo huku akiwa anacheka jambo linalomaanisha ni utani.