RIHANNA AOMBA KUPATA SIGN YA MARIAH CAREY KWENYE TITI..

Staa wa Marekani Rihanna hivi karibuni alihudhuria show ya Christmas ya Legend Mariah Carey iliyofanyika Barclays Centre, New York  Marekani, Mariah Carey alionekana kurudi nyuma kidogo baada ya kugundua kuwa alipishana na Rihanna wakati anasalimia mashabiki zake waliokaa VIP.

Baada ya kurudi Carey alianza kwa kumtania Rihanna wapi anaweza kupata miwani ya jua kama yake, baada ya hapo Rihanna akaomba sign ya Mariah Carey na alipoulizwa asaini wapi kwenye nguo ama sehemu gani, Rihanna alichagua upande wa titi la kushoto ulipo moyo. Na wakati anasaini alikua mwenye furaha na kusema kuwa Waoo This is ICONIC akimaanisha kufurahia kupata Saini ya Mkongwe, Mariah Carey alipouliza unataka niandike nini Rihanna akajibu chochote.

Baada ya kuwekwa Saini ya mariah Carey, Rihanna akawaonyesha watu akisema ‘Angalieni nyinyi wote, Nakupenda Carey’  –  Rihanna.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *