Rais wa chama cha soka Hispania (FA) Luis Rubiales amethibitisha kuacha/kujiuzulu kuwa Rais wa Shirikisho la Spain kufutia tuhuma zinazomkabili dhidi ya Kiungo wa Spain, Jenni Hermoso kwa kumbusu Hadharani bila ruhusa yake.
Tukio hilo liliotea siku ya fainali ya Kombe la Dunia la Wanawake baada ya Ushindi wa Hispania dhidi ya Uingereza. Hat hivyo Rubiales amedai kuwa busu hilo lilikuwa la kuheshimiana tu.
Hata hivyo mwanadada Hermoso amesema busu hilo alilopigwa na Rais huyo halikuwa la makubaliano kati yao na tayari alishawasilisha Madai ya kisheria.