Rhoda aua watoto wake mapacha

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Roda Peter (30) Mkazi wa Kihonda mkoani humo kwa tuhuma za kuua watoto wake pacha, wenye jinsia ya kike na kiume, wanaokadiriwa kuwa na umri wa siku moja.

Jeshi la polisi limedai kuwa baada ya kujifungua, mwanamke huyo aliviweka vichanga hivyo kwenye mifuko miwili ya salfeti yenye rangi nyeupe na nyeusi kisha kuvitupa kwenye vichaka. Pacha hao walikutwa wakiwa wamefariki dunia.

Mtuhumiwa alitenda kosa hilo Oktoba 12 mwaka huu maeneo ya Kihonda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *