Kutoka Mavin Records, kijana wa miaka 23, Rema anaingia kwenye historia ya kuujaza ukumbi wa O2 Arena huko nchini Uingereza, usiku wa kumkia leo katika shoo yake ya ‘Rema- Ravage Uprising’

Rema anaungana na mastaa kama Davido, Wizkid, Burna Boy, na Asake kuuza tiketi zipatazo 20,000 na kupelekea ukumbi huo O2 Arena kufurika.
Tamasha la Rema la O2 Arena ni uthibitisho wa hadhi ya nyota tano katika muziki wa Afrobeats, na pia ni tamasha lilojawa upendo kwani alitoa nafasi kwa Ayra Starr pia kukiwasha jukwaani, kama ambavyo pia Burna Boy alivyowahi kufanya juu yake. Hata hivyo unaambiwa siku ya jana pia Burna Boy akiwa na washikaji zake walitulia sehemu kutazama Live shoo ya kijana huko kutoka Benin.