Red Tabara Wazigonganisha Rwanda na Burundi

Serikali ya Rwanda imekanusha madai ya Burundi kwamba iliwapa silaha waasi wa Red-Tabara kupitia taarifa iliyotolewa siku moja baada ya Burundi kuishutumu Rwanda kwamba imewapa mafunzo na silaha waasi wanaolaumiwa kwa mashambulizi mawili ya guruneti yaliyosababisha majeruhi ya Watu 38 katika shambulizi lililofanyika ijumaa katika mji mkuu wa Burundi Bujumbura.

Msemaji wa serikali ya Rwanda Yolande Makolo, amekanusha madai hayo, akisema hayana uhusiano kabisa na shambulio hilo,Makolo amesema Burundi ina tatizo na Rwanda, lakini wao hawana tatizo na Burundi  na kuwataka viongozi wa Burundi kutatua matatizo yao ya ndani bila kuihusisha Rwanda.

Uhusiano kati ya nchi hizo mbili jirani, mara kwa mara umekuwa wa kupanda na kushuka na Burundi imekuwa ikiishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi hao,madai ambayo yamekanushwa na Serikali ya Rwanda na pia kundi hilo la Red-Tabara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *