Na Costantine James,Geita
Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amewataka wafanyabiashara na wajasiriamali mbalimbali wanawake Mkoani Geita kuchangamkia fursa za masoko ya bidhaa zao mbalimbali wanazozalisha katika soko la Afrika Mashariki hali itakayowawezesha kujiimarisha na kujitanua kiuchumi na kujulikana kimataifa zaidi.
RC Shigela ameyasema hayo leo (Juni 19,2024) wakati akizungumza na wanachama wa Chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Mkoa wa Geita katika mafunzo yaliyowakutanisha wajasiriamali na wafanyabiashara kutoka Wilaya za Mkoa wa Geita amesema serikali inahitaji nguvu za ziada kutoka katika sekta binafsi hivyo wafanyabiashara wanapaswa kuchangamkia fursa hasa kimataifa.
Rais wa chama wa Chama cha wanawake wafanyabiashara Tanzania (TWCC) Taifa Bi. Mercy Sila akatumia nafasi hiyo kuiomba Serikali kuanza kutekeleza Sheria ya Manunuzi iliyotungwa na Bunge ya kuzilazimisha taasisi nunuzi kutenga asilimia 30 ya manunuzi yao kwa ajili ya makundi maalumu ya wanawake,vijana na wenye ulemavu lengo ni kuyapa fursa mbalimbali makundi hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema Chama cha Wanawake wafanyabiashara Tanzania (TWCC) kimekuwa msaada kwao katika kuwapa mafunzo wajasiriamali na wafanyabiashara mbalimbali ambayo yamekuwa masaada kwao kuwafungalia fursa za masoko hasa kimataifa.