RC MRINDOKO ATAKA MIRADI ITAKAYOPITIWA NA MWENGE TANGANYIKA IKAMILIKE

Na Daniel Gahu – Katavi.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko ameelekeza ukamilishwaji wa miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ambapo Mwenge wa Uhuru utapokelewa Kimkoa na kisha kukimbizwa Mkoa Mzima.

Katika ziara yake ya kikazi wilayani Tanganyika yenye lengo la kuangalia maadalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, Mhe Mrindoko ameambatana na Kamati yake ya Mwenge Kimkoa, Wilaya na Taasisi zote, ameridhishwa na maandalizi yanayofanywa na Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika ikiwemo ukamilishwaji wa miradi na nyaraka zake zote zinazotakiwa kuwepo.

Sambamba na ziara hiyo iliyoenda sawia na ufanyaji wa hamasa kwa wananchi wa maeneo yote, hususani yale ambayo yatakayopitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru na maeneo jirani. Mheshimiwa Mrindoko amewataka wananchi wote wa Mkoa wa Katavi kushiriki kwa amani katika uchaguzi mkuu Oktoba 29, 2025. 

“Niwatake wananchi kujitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge wa Uhuru na sambamba na hilo tunafahamu kwamba mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi, hivyo Mwananchi usikubali kuuza kitambulisho chako kitunze vizuri ili umchague kiongozi unayeona anafaa kukuletea maendeleo, na katika zoezi hilo nawaomba sana mshiriki kwa amani na utulivu,” RC Mrindoko.

Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika utatembelea miradi mitano, ambayo ni Mradi wa maji Kijiji cha Mazwe, Mradi wa Zahanati ya Vikonge, Ujenzi wa Barabara za lami Kilomita nne za Majalila, Bweni la Wasichana Sekondari ya Majalila na Kikundi cha Bodaboda na Samia kilichonufaika na mkopo wa asilimia kumi kutoka Halmashauri hiyo.

Pia Mwenge wa Uhuru utatembelea klanu ya Lishe Luhafwe, Klabu ya Kupambana na Kuzuia Rushwa zote za ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika na kisha mbio hizo za Mwenge wa Uhuru kikimbizwa katika maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa wa Katavi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *