Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mh.Christina Mndeme akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa hii leo Novemba 21,2023 amefanya ziara ya utalii wa viwanda katika kiwanda cha Jambo Food Products kilichopo Ibadakuli mkoani Shinyanga.
Kupitia ziara hiyo akiongozwa na Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya Jambo Food Products Bw.Salum Khamis Salum,RC Mndeme amejionea shughuli mbalimbali za uzalishaji wa bidhaa za kampuni hiyo na kufanya mazungumzo ya kuimarisha uhusiano uliopo kati ya serikali na mwekezaji huyo.