
NA EUNICE KANUMBA –SHINYANGA
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita leo amefungua mafunzo ya siku mbili kwa wajumbe wa kamati za maadili za maafisa wa mahakama za wilaya na mkoa yenye lengo la kuwajengea uwezo wajumbe hao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi.
Akizungumza wakati akigungua mafunzo hayo kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga RC Mboni amesema kamati za maadili ndiyo nguzo na msingi wa chombo cha mahakama katika kusimamia utoaji wa haki na uwajibikaji
RC Mboni amesema mafunzo hayo yana umuhimu mkubwa sana kwasababu yanatoa fursa ya kuwajengea uwezo wajumbe hao wakamati za maadili na kwamba ana imani watakwenda kulinda haki na umanifu ili kulinda hadhi ya muhimili wa mahakama.
RC Mboni ameongeza kwa kusema maadili bora ndiyo nguzo ya haki ya na msingi kwani wananchi wamekuwa na imani kubwa kwa chombo cha mahakama huku akianisha kwamaba bila maadili heshima na thamani ya mahakama ubaki mashakani.
“Nataka kuona kamati za maadili zinakuwa chombo cha kuimarisha nidhamu na uwajibikaji na hatimae kujenga taswira chanya ya mahakama kwa wananchi weti “ amesema RC Mboni.

Naye Naibu katibu wa tume ya utumishi wa mahakama anayesimamia maadili Alesia Mbuya amesema ili kuweka uwakilishi kwa makundi yote katika kamati hizo, zimejumuisha viongozi wa dini, viongozi wa serikali, wawakilishi wa wananchi pamoja na mahakimu lengo likiwa ni kuhakikisha maamuzi yanayofikwa yanakuwa na masilahi ya pande zote mbili
“Ili kamati hizi ziweze kufanya kazi kwa ufanisi na weledi tume imeona umuhimu wa kuwa na mafuzno ya mara kwa mara kwa ajili ya kuwajengea uwezo wajumbe wake “amesema Mbuya
Awali wajumbe wa kamati hizo walikula kiapo kutumikia na kutunza siri za kamati hizo kilichosimamiwa na jaji wa mahakama kuu kanda ya Shinyanga Ruth Masam ambapo amewataka wajumbe hao kusikiliza kwa makini mafunzo watakayopatiwa kuhusiana na mwongozo wa kanuni za uendeshaji kamati za maadili za wilaya na mkoa.



