RC MAKONGORO ATAKA UKAGUZI FEDHA ZA MIRADI YA UJENZI RUKWA

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere amewaagiza wakuu wa TAKUKURU katika Wilaya za Nkasi na Sumbawanga, kuchunguza matumizi ya fedha katika mradi wa Shule ya Sekondari ya Wachina na ujenzi wa shule mpya ya amali ya mkoa.

Makongoro pia ametaka kupokea taarifa ndani ya siku 14, kufuatia kutoridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wa baadhi ya majengo, katika miradi hiyo muhimu ya kielimu mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere.

Katika ziara yake ya hivi karibuni, ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kwenye wilaya tatu za mkoa huo, RC Makongoro amesisitiza kuwa miradi yote, ukiwemo wa shule ya Sekondari ya amali, lazima ikamilike ndani ya siku 30.

Hatua hiyo, inalenga kuhakikisha thamani ya fedha za Serikali inaonekana na Wananchi wanaanza kunufaika na miundombinu hiyo mipya ya elimu na mafunzo ya ufundi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *