
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza C.P.A Amos Makalla ambaye ni mlezi wa timu ya Pamba Jiji Football Club amekoleza moto kwenye mchezo wa timu hiyo dhidi ya Biashara United Jumapili hii kwenye uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, kwa kutoa motisha ya Shilingi Milioni 5 kwa wachezaji na benchi la Ufundi.
Mbali na motisha hiyo lakini pia amekunywa nao chai ya asubuhi na kuwatakia kuwa na Mchezo mwema kwa kutambua alama tatu ndiyo lengo Muhimu Ili kujiweka vizuri kwenye msimamo wa NBC championship.
Aidha ametamba kuwa hawezi kushindwa na wanajeshi wa mpakani kwani kazi yao ni moja tu kulinda mipaka ya nchi lakini Boli waliachie Pamba Jiji FC.