RC Macha:Serikali Inatambua Mchango wa NGO’s

Mkuu wa Mkoa wa ShinyangaAnamringi Macha amesema kuwa Serikali inatambua na kuthamini sana kazi zote zinazofanywa na Mashirika mbalimbali yasiyokuwa ya Kiserikali nchini.
RC Macha ameyasema hayo kaupitia mazungumzo na Viongozi mbalimbali wa World Vision Kanda ya Ziwa wakiongozwa na Meneja wa Kanda Bi. Jacqueline Kaihura waliofika ofisini kwake ambapo pamoja na mambo mengine amewaahidi ushirikiano kutoka Serikalini wakati wote huku akiwapongeza kwa namna wanavyotekeleza miradi yao ambayo inagusa maisha ya wananchi wa Shinyanga na maeneo mengine nchini.

“Napenda kuwaambia kwamba, Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua, inathamini kazi zote mnazozifanya World Vision Kanda ya Ziwa na jwa muktadha huu Serikali itaendelea kufanya kazi nanyi wakati wote, hongereni sana na karibuni tena Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,” amesema RC Macha.

Uongozi wa World Vision Kanda ya Ziwa wamefika Ofisini kwa RC Macha kwa lengo kujitambulisha kwake na kueleza shughuli mbalimbali zinazotekelezwa katika Kanda hii ya Ziwa ambayo inajumuisha Mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Tabora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *