Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

RC Macha Kuzindua Safari ya Jambo Fm Kuwa Benki

Na Ibrahim Rojala

Kueleka katika ufunguzi rasmi wa Jambo kuwa Benki leo hii Mei 15,2024, kwa heshima kubwa Mgeni rasmi wa Safari ya Jambo kuwa Benki ni Mhe.Anamringi Macha Mkuu wa mkoa wa Shinyanga.

Jiandae kutuma na kupokea miamala na huduma nzuri kutoka Benki yetu yenye lengo kubwa la kukupatia Maisha fresh kila siku kupitia kwa huduma bora na salama zaidi, kila siku mambo yako freshi karibu tukuhudumie leo hii , Kuanzia Saa 6:Mchana hadi saa 10:00 Jioni usikose.

Kuelekea Maandalizi ya Siku hii Muhimu,hapo jana kupitia mazungumzo Maalum aliyoyafanya na Meneja Mkuu wa Jambo Media Bw. Nickson George akiwa ofisini kwake,Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha ameipongeza Kampuni ya Jambo Group of Companies kwa uamuzi wa kuwekeza katika mkoa wa Shinyanga akielezea kwamba uwekezaji huo umefungua fursa mbalimbali ikiwemo ajira.

RC Macha ameelezea kuridhishwa na kuutambua mchango wa Jambo Group ambao umekwenda mbali zaidi hadi katika sekta ya Michezo kwa kuwezesha udhamini kwa timu ya Stand United.

“Kwa Shinyanga,Specific kwa wilaya ya Shinyanga ambayo ndio makao makuu ya mkoa hakuna development ya viwanda na mtu anaweza kuja kuangalia mazingira ya hapa na akawa na mashaka kuweka viwanda lazima tukiri ni mji mzuri sana lakini haujawa very well combined katika viwanda,hakujawa na bishara nyingi za kutosha as a kiwanda lazima tuone Jambo as Giant Industries kama kampuni yenye viwanda vingi hivyo tupongeze na ndani ya viwanda hivi kuna ajira na kuna mapato ya Serikali”Amesema RC Macha.

Akizungumza kuhusiana na ushirikiano na jamii pamoja na kujali wafanyakazi,RC Macha amesema kutoa zawadi kwa wafanyakazi kupitia sikukuu ya Mei Mosi,malipo ya stahiki za wafanyakazi kwa utaratibu unaostahili,kuzingatia usalama wa wafanyakazi ni mambo yanayopatikana katika viwanda vichache vya binafsi na ni kielelezo cha utendaji bora na kuahidi kushirikiana na Jambo Group katika kuhakikisha timu ya Stand United inaendelea kuwepo akiamini kwamba timu hiyo ikisimamiwa vizuri na kuwa na uongozi imara itawezesha kuuchangamsha mkoa.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa Wa Shinyanga amepongeza aina za Programu zinazoendeshwa na Jambo Media kutokana na maudhui yake kuwalenga vijana akieleza kuwa kundi hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali zilizozababishwa na Mtindo wa maisha ambazo ni pamoja na matatizo ya Kiafya,Kushindwa kutofautisha kati ya ajira na kazi pamoja na tamaa za mafanikio ya muda mfupi na uwepo wa kasumba ya kudharau baadhi ya kazi ikiwemo kilimo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *