RC MACHA AZINDUA RASMI VITAMBULISHO VYA WASIIONA SHINYANGA.

NA EUNICE KANUMBA –SHINYANGA 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,  Anamringi Macha, amezindua rasmi vitambulisho vya kisasa vya kielektroniki kwa wanachama wa Chama cha Wasioona Tanzania (TLB) katika mkutano mkuu wa kitaifa wa chama hicho uliofanyika mkoani humo.

Uzinduzi huo umefanyika leo Juni 17, 2025 kama sehemu ya jitihada za kuimarisha utambuzi, usalama na heshima ya watu wenye ulemavu wa kuona, sambamba na kuwasaidia kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na kiuchumi. Mkutano huo umehusisha wanachama kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Akizungumza katika uzinduzi huo, RC  Macha amesema Serikali inatambua mchango wa watu wenye ulemavu katika maendeleo ya taifa na kwamba matumizi ya teknolojia ni njia mojawapo ya kuwawezesha kufikia fursa mbalimbali kwa usawa.

“Vitambulisho hivi vya kisasa vitawawezesha wanachama wa TLB kutambulika kwa urahisi na kupata huduma muhimu kwa heshima wanayostahili. Serikali itaendelea kushirikiana.

Kwa upande wake, Habiba Salum Mwenyekiti wa chama cha wasioona Tanzania TLB amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuonesha ushirikiano na kuahidi kuvitumia vitambulisho hivyo kwa ufanisi ili kukuza uwajibikaji na ushirikiano ndani ya chama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *