RC Macha Asema “Mwambie Don’t Touch Me”

Na Eunice Kanumba,Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha amewataka wanafunzi wanaoshiriki michuano ya michezo kwa shule za msingi (UMITASHUMTA) kuwa makini na kukataa kufanyiwa vitendo viovu na vya kikatili pindi waonapo dalili za mtu yeyote kutaka kuwafanyia vitendo hivyo na wawe tayari kutoa taarifa katika mamlaka husika.

Rc Macha ameyasema hayo Leo Juni 4,2024 wakati akifunga kambi ya mkoa ya UMITASHUMTA pamoja na kuwaaga wanafunzi 120 ambao wanaelekea mkoani Tabora kuuwakilisha mkoa katika mashindano hayo ngazi ya Taifa ambayo yanaanza kutimua vumbi Juni 5,2025 ambapo pia amewataka Wakurugenzi katika Halmashuri zote kutenga maeneo ya michezo kwa watoto shuleni pamoja na kuzuia uvamizi katika viwanja hivyo.

Awali akitoa taarifa ya hali ya michezo katika mkoa wa Shinyanga afisa elimu mkoa huo Mwalimu Dafroza Ndalichako ameleezea changamoto wanazokumbana nazo katika suala zima la uendeshaji wa michezo mashuleni kuwa ni pamoja na ufinyu wa bajeti hali inayopelekea upungufu katika upatikanaji wa vifaa vya michezo

Akizungumza kwa niba ya wanafunzi wanaokwenda katika mashindano hayo Grace Boazi kutoka katika halimashuri ya Msalala ameahidi kwenda kufanya vizuri na kurudi na ushindi huku mwalimu Nyarusana Chacha akiahidi kuwalinda watoto katika siku zote watazokuwa kambini mkoani Tabora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *