Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

RC Macha amewataka wasukuma kuachana na mila zinazochochea ukatili wa kijinsia

Jamii ya kabila la Wasukuma Mkoani Shinyanga imetakiwa kuachana na mila potofu zilizopitwa na wakati ambazo zinachochea ukatili wa kijinsia badala yake waendeleze zile zilizo nzuri zenye kuleta umoja,mshikamano na Amani miongoni mwa wanajami
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha wakati akitoa salamu zake kwenye hafla ya kimila ya ufanyaji tambiko na kusherehekea msimu wa mavuno na kujiweka tayari katika msimu ujao wa kilimo iliyofanyika katika makazi ya chifu wa eneo la kimila la busia yaliyoko katika kata ya ukenyenge wilayani kishapu.

Naye kiongozi wa kimila Chifu Muli kutoka jamii ya ukoo wa Anzaoni katika kauti ya kituli iliyopo nchini Kenya amesema amefurahishwa sana kukuta katika jamii hiyo ina vijana wadogo wanaojihusisha na masuala ya utamaduni tofauti na hali ilivyo nchini Kenya ambapo wanajiohusisha zaidi na masula ya utamaduni ni wazee pekee.

Naye chifu wa kabila la Wasukuma Mkoani humo anayeongoza koo ya Busiha ametumia jukwaa hilo kuitaka jamii kujitokeza kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu ili kuchagua viongozi wenye weledi ambao wanasikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Aidha Baadhi ya machifu katika koo mbalimbali zilizopo katika jamii ya wasukuma wameiomba serikali kuthamini hafla hizo za jadi kwani zimekuwa msaada mkubwa katika malezi ya vijana katika kuziishi mila na destri zao hususani katika kupindi hiki cha utandawazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *