Rayvanny na Diamond Platnumz walitaka kuomba uraia wa Kenya

Staa wa muziki Rayvanny ameweka wazi kuwa mwaka 2018 baada ya kufungiwa na BASATA, kufanya shoo ndani na nje ya Nchi yeye na Diamond kwa muda usiojulikana, walipanga kuomba uraia wa nchini Kenya.

Rayvanny amefunguka hayo kupitia mahojiano aliyofanya nchini Kenya kupitia Radio Citizen.

Utakumbuka Disemba 18, 2018, BASATA walifungiwa wasanii hao ambao walikuwa chini ya lebo ya WCB, baada ya kufanya matendo yasiyo ya maadili na wakati huo wimbo wa ‘Mwanza’ ulitoka na walitumbuiza juklwaani ilihali walikuwa wamekatazwa.  

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *