Aliyekua memba wa Familia ya WCB Wasafi ambaye kwa sasa ni Rais wa Next Level Music, Rayvanny amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya kuonekana kwa picha ya Diamond na Harmonize kwenye futari ya Rais Samia.
Rayvanny amesema ‘Kila hatua ya Mafanikio ya Mwanadamu ina chanzo chake !!! Lakini sisi binadamu huwa hatuwezi shindwa kupishana au kukosana na Hasa yanapotokea Maneno na changamoto tofauti tofauti za Kimaisha !!! Ilikua haina ulazima kuweka picha hii kwenye siku yako ya kuzaliwa ila hii nimeweka ikiwa ni sehemu ya Furaha
kwangu kuona AMANI ipo Kati Yenu FAMILIA YANGU’ – Rayvanny
‘HAPPY BIRTHDAY KONDE BWAY ENJOY YOUR BIG DAY BROSKI FAMILY FOREVER’ – Rayvanny