RASMI MOUSA BALLA CONTE NI MWANANCHI

Mchezaji wa soka kutoka Nchini Guinea, Moussa Balla Conte ametambulishwa rasmi kuwa Mchezaji mpya wa Yanga SC akitokea CS Sfaxien ya Tunisia.

Kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii, Yanga SC imethibitisha kuipata saini ya kiungo huyo.

Usajili wa Conte ulizua utata kufuatia ripoti za awali kumhusisha kiungo huyo kuwa mawindoni mwa mahasimu wao Simba SC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *