Kikundi cha sarakasi kutoka Tanzania cha Ramadhani Brothers kinachoundwa na Fadhili Ramadhani na Ibrahim Jobu, wametinga kwenye Fainali za America’s Got Talents. Fainali hizo zinafantika nchini Marekani wiki ijayo.
Mwaka 2022, kikundi hicho kilifanikiwa kufika fainali ya msimu 17 wa La France a Un Incroyable Talent. Pia Australia’s Got Talent walipata Golden Buzzer kutoka kwa Kate Richie.
Kwa mwaka huu 2023, walifika nusu fainali ya msimu wa 13 wa Romani. Pia walifika fainali za ‘The Champions’ inayojulikana kama Got Talent All-Stars ya Uhispania.