Good news wiki hii kutoka Tanzania ni ushindi wa Watanzania, Fadhili na Ibrahim (Ramadhani Brothers) ambao wameibuka na ushindi kupitia American Got Talent fantasy league ambapo wamejishindia Dola 250,000 sawa na zaidi ya Shilingi Milioni 600 za Kitanzania.

Sehemu kubwa ya mjadala imekua ni suala la kodi ya ndani, ambapo Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA wameona mjadala huo na wamewajibu Wananchi waliotaka kujua kama kuna mapato yoyote Ramadhani Brothers watalipa kwao, kupitia Instagram TRA wameandika ‘Kwa aliye na sifa za mkazi wa Tanzania analipa kodi ya mapato atakayopata popote duniani. Na kwa kuwa hawa ni watu binafsi watalipa kodi kulingana na kiwango cha mtu binafsi ambacho ni shilingi 1,536,000 kujumlisha 30% ya kiasi kinachozidi milioni’

‘Na hiyo ndiyo kodi watakayolipa kila mmoja kulingana na vipato watakavyopata baada ya kutoa gharama. Hakutakuwa na 10% ya nyongeza kwa kuwa hawana repatriated income. Pia wanaweza kupata unafuu wa kodi hapa Tanzania kwa kulingana na kifungu cha 77 cha sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004’ – TRA.