Rais wa Romania kuanza ziara nchini kesho

Rais wa Romania, Klaus Iohannis, anatarajia kufanya ziara ya Kitaifa nchini kuanzia kesho Novemba 16 hadi 19, 2023 kwa mwaliko wa Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan lengo likiwa ni kukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Romania pamoja na kuibua maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta mbalimbali kama Uwekezaji, Elimu, Utalii, Afya na Utamaduni.

Kupitia ziara hii Tanzania na Roamania zimedhamiria kuinua na kuimarisha kiwango cha biashara kati ya Nchi hizi mbili ambacho licha ya Tanzania kuuza zaidi bidhaa zake nchini Romania, kiwango cha biashara kati ya mataifa haya mawili bado ni kidogo na kimeshuka katika miaka ya hivi karibuni ikilinganishwa na fursa za kibiashara zilizopo.

Uhusiano wa Kibiashara na Uwekezaji Tanzania na Romania zimeendelea kushirikiana katika sekta ya biashara na uwekezaji ambapo bidhaa kuu za Tanzania zinazouzwa Romania ni minofu ya samaki aina ya sangara, chai, tumbaku na parachichi, Tanzania pia inanunua kutoka Romania bidhaa za mashine za umeme, vifaa vya matrekta, magari na vifaa vya matibabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *