Rais Tshisekedi kuapishwa leo

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Felix Tshisekedi anatarajiwa kuapishwa leo kuliongoza Taifa hilo kwa muhula wa pili, hafla ambayo inafanyika jijini Kinshasa huku kukiwa na vuguvugu la upinzani.

Mwakilishi mkuu wa Tshisekedi, Serge Tshibangu, amesema marais 18 wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo wakiwemo makamu wa rais wawili, pamoja na marais wastaafu wanne.

Hata hivyo, upinzani unaendelea kudai matokeo ya uchaguzi huo uliompa ushindi Tshisekedi sio yake na yanafaa kufutwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *