RAIS TSHISEKEDI AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, amewasili Zanzibar kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, Agosti 17–18, 2026, kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akiwa nchini, Rais Tshisekedi anatarajiwa kufanya mazungumzo na Rais Samia kuhusu kuimarisha ushirikiano wa Tanzania na DRC katika biashara, uwekezaji, madini, nishati, miundombinu, kilimo, afya na teknolojia ya kidijitali.

Viongozi hao pia wanatarajiwa kujadili amani na usalama katika ukanda wa Maziwa Makuu pamoja na masuala ya kikanda na kimataifa yenye maslahi ya pamoja.Samia Suluhu Hassan Ikulu Tanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *