RAIS SAMIA KUZINDUA MPANGO WA KITAIFA WA CHANJO ZA MIFUGO.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Samia Suluhu Hassan anatarajia kubariki uzinduzi wa Mpango wa Kitaifa Wa Chanjo za Mifugo, uzinduzi muhimu uliyopangwa kufanyia Tarehe 16, mwezi huu katika viwanja vya Nyakabindi vilivyopo Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.

Hafla ya uzinduzi wa Mpango huo unaotarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano (2024-2029), huku likitanguliwa na Kongamano maalamu la wafugaji nchini Tanzania.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Chama Cha Wafugaji Tanzania litafanyika kwa siku mbili mfululizo, Tarehe 14 na 15, na litafunguliwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dr. Emmanuel Nchimbi.

Akiongea na waandishi wa habari Jijini Dodoma leo, Junatano Juni 11,  2025, Waziri wa Mifugo, Dkt Ashantu Jijaji amesema Mpango Mpango wa Kitaifa Wa Chanjo za Mifigo unaakisi juhudi za Serikali kuboresha sekta ya Mifugo nchini Tanzania, haswa katika kuwezesha Tanzania kunufaika na masoko makubwa ya bidhaa za nyama nje ya Nchi .

“Tanzania tumebarikiwa kuwa na azina kubwa ya miifigo mbalimbali, lakini Nchi inashindwa kunufaika na masoko ya nje ya Nchi Kwa sababu ya uwepo wa magonjwa mbalimbali ya Mifugo,” Waziri Dkt. Kijaji amesema.

Amesema, kupitia utekelezaji wa mkakati huo wa chanjo unatarajia kugharimu angalau Shilingi Bilioni  216, Serikali inatatajia kupanua kiwango cha usafirishaji wa nyama kutoka tani 14,000 kwa sasa,  hadi kufikia tani 30,000 ifikapo mwaka 2029.

Aidha, amesema ongezeko hilo la usafirishaji wa nyama nje ya Nchi linalotarajiwa, litaiwezesha Nchi kuingiza kiasi cha Dola za Kimarekani 152,287,305.2, kutoka Dola 51,894,622, ambazo Nchi zinapata kwa sasa.

Amesema, mkakati huo unatarajia kuchanja angalau asilimia 70 ya Mifugo yote Tanzania.

“Katika awamu ya kwanza, ng’ombe 19,097,223 wanatarajia kupewa chanjo katika maeneo mbalimbali ya nchi,” Waziri alifafanua.

Aliongeza kuwa, katika chanjo hiyo ya kitaifa inayokaribia, jumla ya mbuzi 20, 900,000 watachanjwa dhidi ya magonjwa mbalimbali.

“Zoezi hili la chanjo litahusisha pia sekta ya kuku, ambapo jumla ya kuku wa kienyeji 40,000,000 watachanjwa,” Waziri Dkt. Kijaji aliongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *